Niliacha kazi kufanya mziki Wakatabiri ntalosti Wengine wakashawishi tuloge kuondoa mikosi Nakomaa na mziki ingawa jua la utosi Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi Jina langu lisha tumika sana kutajilisha watu Nyota ndogo asha sema kuna watu na viatu Bunduki haiui watu ila watu ndo wanau watu Dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu Ni saa mbaya Watu wana husda na roho mbaya Tunawaita watakatifu kumbe ni mavimpire Yalisemwa mengi Demu wangu alipo toroka Ni fundisho tosha Na changamoto kwa mwana choka Nimepitia mengi mitihani ya kila namna Ndo maana sishangai wakiniita mbeba lawama Washikaji wengine feki kwenye shida hawakujui Wanazani kila jogoo akiwika niasubuhi. Liziki hamwezi ziba Labda mtaichelewesha tuu Mnakesha mnanishusha mwenyezi ananipaisha Kote mliko bana Kidume ndo natusua Mnanijua nakamua Roho za wanga zinaungua. Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Nami nishike mkono nishinde Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Mwanachonga daima nishindwe Walisha zusha nimekua Eti nimepata ajari Washindwe na walegee Mweyezi niepushe mbali Wakasema nina ukimwi Kwakua nilikonda ghafla Wanataka kunizika mzima kabla sijafa Walo sema nina ngoma Wengine tusha fukia Wanaomba nife leo Naamini watatangulia Mama pumzika pema Daima tunakulilia Na bado wanachonga sana But men the king is here Daima mtaji wangu Ni nguvu zangu mwenyewe Simwamini mtu kamwe Najiamini mi mwenyewe Hata nikinwya maji Wanadai nakunywa pombe Mi sijali I knock them all Wanalizombe Bado tunapigana Kibarua kisiote nyasi Daima sito wadhuru Wale wote walio niasi Nikikaa kimya Msizani sijasikia Sio bahati Sio ngekewa Ni sauti ilio barikiwa Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Nami nishike mkono nishinde Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Wanachonga daima nishindwe Mungu walaze pema Waliisema kajiua Ingawa wote tunapita Naamini maisha ni hatua Maneno ya watu sumu Yanaponya na yanaua Pliz nipe ujasiri Mpaka siku ukinchukua Wape nguvu wale wote walio kata tamaa Maneno yanaleta hila na mizozo kwenye mitaa. Wanaesabu mabaya tuu Na mema hawayaoni Wanakuchekea machoni Wanakuloga moyoni Wanacheka chinichini Wakati una msiba Wakwanza kukutangaza Kwa watu ukiwa na shida. Wantamani wapangue Kila mora alicho panga Wanatangaza amani Huku wameshika mapanga Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Nami nishike mkono nishinde Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde Kwenye hii vita mie Wanachonga daima nishindwe Thai... Mi maneno nsha zoea (aaaah) Ndo maana sijali wanapo ongea (aaah eeeeh) Wanasema maneno mengi mengi mengiiii... Ehieh